Jarida la Kilimo, Julai - Septemba, 2011
Jarida la Kilimo, Julai - Septemba, 2011
Jarida la Kilimo, Julai - Septemba, 2011
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
Toleo la Saba

ISSN: 1821-8113 Julai - Septemba, 2011

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe: Dkt. Ali Mohamed Shein wa pili

kutoka kushoto pomoja na viongozi wengine akiwa katika harakati za uvunaji wa mpunga wa

mbegu aina ya NERICA kituo cha uzalishaji wa mbegu Bambi, Wilaya ya Kati Unguja.

Yaliyomo

Maoni ya Mhariri/Picha ya Jalada...........................................................................Uk.2

Uvunaji na Uanikaji wa Karafuu............................................................................Uk.3 - 4

Upotevu wa Rutuba na Urutubishaji wa Ardhi.......................................................Uk.4 - 5

Uvunaji na Uanikaji wa Karafuu..............................................................................Uk.6 - 7

Matukio katika Picha.............................................................................................Uk.8 - 9

Mabaraza ya Wakulima..........................................................................................Uk.10

Athari za Joto kwa Mifugo...............................................................................Uk.11 - 12

Mbinu Bora za Ujasiriamali..............................................................................Uk.13 - 14

Umuhimu wa Rasilimali za Msituni......................................................................Uk. 15 - 16
Julai - Septemba, 2011 WAHARIRI/MAONI/PICHA YA JARIDA

Bodi ya Wahariri MAONI YA MHARIRI

Washauri

Affan O. Maalim

Juma Ali Juma

Dk. Bakar S. Asseid

Mhariri Mkuu

Dk. Juma M. Akil

Msanifu na Mhariri

Mtendaji

Hashim H. Chande

Wahariri Wasaidizi

Makame M. Abdulrahman

Nassor S. Mkarafuu

Nassor S. Mohammed

Mpiga chapa

Fatma A. Juma

Mpiga picha

Khamis A. Bakari

ANUWANI

Wizara ya Kilimo,

Maliasili - Zanzibar

S.L.P. 159

Simu: +255 24 2230986

Fax: +255 24 2234650

E-mail: kilimo@zanlink.com

Tovuti: kilimoznz.or.tz

Ndugu wakulima, kupata chakula cha kutosha na kilicho

bora kwa kila mwananchi ni suala gumu ambalo linahitaji

mipango na mikakati mizuri ya serikali kupitia Wizara

husika. Moja ya tatizo kubwa linalowakabili wananchi ni

kuchelewa kukamilisha hatua za mwanzo za matayarisho ya

mashamba, kulima eneo kubwa ambalo hawana uwezo nalo

na kutokutumia zana na pembejeo bora za kilimo.

Ndugu wakulima, moja ya kikwazo kikubwa ni uwezo mdogo

wa kutumia zana bora za kilimo, mbegu bora, mbolea na

kutozingatia kanuni na taaluma bora za uzalishaji ambazo

zinatolewa na Wizara ya Kilimo na Maliasili. Vikwazo hivi

humsababishia mkulima kutumia nguvu nyingi, muda

mrefu na kupata mavuno hafi fu na tija ndogo.

Ndugu wakulima, kwa miaka mingi neno “Ukulima wa

Kisasa” limekuwa ni wimbo lakini bado mkulima wa visiwani

anategemea zana na pembejeo duni kama vile mbegu na

jembe la mkono (kijembe kongoroka). Serikali ya Mapinduzi

ya Zanzibar kupitia Wizara ya Kilimo na Maliasili inafanya

mabadiliko makubwa katika kilimo ili kukifanya kilimo hicho

kiwe katika mfumo wa kisasa “Mapinduzi ya Kilimo”.

Ndugu wakulima, katika kufanikisha suala hili Serikali

imeongeza upatikanaji wa pembejeo na zana za kilimo

yakiwemo matrekta makubwa na madogo, mbegu bora na

mbolea, kuongeza usamabazaji wa taaluma kwa wakulima

kwa kuongeza idadi ya mabwana/mabibishamba katika

shehia pamoja na kutoa ruzuku ya aslimia 75% kwa kazi za

utayarishaji wa mashamba na ununuzi wa mbegu bora na

mbolea.

Ndugu wakulima, hatunabudi kuunga mkono juhudi hizi

za Serikali ili kufanikisha azma ya “Mapinduzi ya Kilimo”

hivyo tunaipongeza na tunaiomba iendelee na juhudi zake

za kuwashajiisha na kuwashirikisha wakulima kikamilifu

katika kupanga malengo yao juu ya mpango wa utumiaji wa

zana na pembejeo bora za kilimo.

Ndugu wakulima, kwa kuunga mkono juhudi hizi za Serikali,

Wizara ya Kilimo na Maliasili itaendelea kutoa mafunzo ya

utumiaji bora wa zana na pembejeo za kilimo na kuweka

mpango maalumu ya mafunzo kwa kila shehia juu ya

umuhimu wa zana hizo pamoja na matumizi yake ili kufi kia

lengo la wakulima katika kujitosheleza kwa chakula, kuinua

hali zao za maisha na kuipunguzia mzigo Serikali wa kuagiza

chakula kutoka nje ya nchi.

PICHA YA JALADA

Katika picha anaonekana Rais wa Zanzibar Mhe. Ali Mohamed Shein

akivuna mpunga wa mbegu aina ya NERICA katika shamba la kuzalisha

mbegu liliopo Bambi pamoja nae kutoka kulia kwake ni Waziri wa

Kilimo na Maliasili Mhe, Mansoor Y. Himid, Mkuu wa Mkoa wa Kusini

(U) Mhe, Mustafa Ibrahim na Naibu Katibu Mkuu (kilimo) ndugu Juma

A. Juma, tarehe 7 Julai 2011.

2
MAZAO BORA Julai - Septemba, 2011

ILI TUVUNE MAZAO BORA NI LAZIMA TUPANDE

MBEGU BORA ZINAZOWEZA KUTUPATIA TIJA

Na Sabiha H. Saleh

Mnamo tarehe 2/7/2011 Rais

wa Zanzibar na Mwenyekiti wa

Baraza la mapinduzi Mhe. Dkt. Ali

Mohammed Shein aliyasema hayo

kwa nyakati tofauti aliposhiriki

kikamilifu katika uzinduzi wa Kitaifa

wa uvunaji wa mbegu ya mpunga aina

ya “NERICA”, huko Bambi na bonde

la Kisima Mchanga liliopo Kiboje

Mkwajuni Wilaya ya Kati Unguja.

Hii ni hatua mojawapo ya Serikali ya

mapinduzi ya Zanzibar katika jitihada

zake za kukuza na kuendeleza kilimo

kwa ujumla.

Dkt. Shein amesema kuwa lengo kuu

la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

kufanya mapinduzi ya kilimo tayari

limeanza kutekelezwa na mbegu

aina ya NERICA ndio mkombozi wetu

kwani Serikali itaendelea kuchukua

kila jitihada kuona kuwa wakulima wa

Zanzibar wananufaika na kilimo chao

pamoja na taifa kwa ujumla.

Alisema kuwa azma ya Serikali kwa

upande wake ni kuona kuwa Mapinduzi

ya kilimo yanaleta tija kwa wakulima

pamoja na wananchi kwa ujumla kwa

kuweza kupata kile kilichokusudiwa.

Aidha, amefahamisha kuwa nia na

dhamira ni kuwainua wakulima na

Serikali inaendelea na taratibu za

kuwaletea wakulima wake mashine

za kuvunia mpunga, kuwapunguzia

bei za pembejeo pamoja na kuwapatia

matrekta kwa ajili ya kuvurugia na

dawa za kuulia wadudu ili mkulima

aweze kumudu gharama za uendeshaji

na tuweze kulima kwa tija zaidi.

Akizungumzia kuhusiana na mfumko

wa bei za vyakula hasa mchele ambao

ndio chakula kikubwa kwa watu wa

Zanzibar amesema kuwa Serikali tayari

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed

Shein aliyesimama na shuke la mpunga akiwa katika uzinduzi wa uvunaji wa mbegu

ya mpunga aina ya NERICA katika Shamba la Uzalishaji wa mbegu Bambi

imeshaanza kutekeleza mapinduzi ya

kilimo kwa kupambana na hali hiyo.

Akifafanua zaidi kuhusu ongezeko la

Idadi ya Watu duniani, kwa upande wa

Zanzibar amesema tokea Mapinduzi

Matukufu ya Januari mwaka 1964

ambapo idadi ya watu ilikuwa 320,000

hadi mwaka 1974 ilikuwa ni 640,000

na kwa mujibu wa takwimu ya sensa

ya mwaka 2002 ambapo ilifi kia watu

milioni 1.2 idadi ambayo inapelekea

ongezeko la mahitaji ya chakula.

Kutokana na ongezeko la watu ,

takwimu zinaonyesha kwamba mchele

unaotumiwa kwa chakula hapa

Zanzibar ni tani 80,000 kwa mwaka,

unaozalishwa na wakulima ni chini ya

tani 16,000 na kiasi chote kilichobaki

hununuliwa kutoka nje ya nchi. Aidha,

Dkt. Shein alisisitiza haja ya kuongeza

uzalishaji wa chakula.

Pia aliwataka wakulima kufuata

ushauri wa watalamu na kubadilika ili

kilimo chetu kiwe cha kisasa. Hivyo,

hatuna budi kutumia teknolojia ya

3

kisasa na kuweza kujitegemea katika

kilimo cha mpunga kwa angalau

asilimia 60, “Ukitumia mbegu bora

unaweza kuvuna mavuno bora”.

Amefahamisha kuwa kulima kwa

kutumia mbegu bora kunapelekea

kuvuna mazao mengi na bora, hivyo

tuongeze jitihada na kukifanya chakula

kuongezeka.

Aidha Dkt. Shein amesema kuwa

Washirika wa Maendeleo wako tayari

na wanaendelea na jitihada za kuiunga

mkono Zanzibar katika Sekta ya Kilimo

wakiwemo, Korea ya Kusini, Marekani,

Japan hasa katika mradi wao wa ‘Feed

the Future’.

Akiwa katika bonde la Kisima

Mchanga, Dkt. Shein aliwaahidi

wakulima kuwajengea njia yao kwa

kiwango cha kifusi kutoka barabara

kuu hadi bondeni, kuwawekea umeme,

kuwachimbia kisima na kuwapatia

trela la kubebea mizigo.

Akimkaribisha Rais wa Zanzibar
Julai - Septemba, 2011 UPOTEVU WA RUTUBA NA URUTUBISHAJI ARDHI

Waziri wa Kilimo na Maliasili Mhe.

Mansoor Yussuf Himid amesema kuwa

Mapinduzi ya Kilimo ni mageuzi ya

haraka yalioendelevu katika kukipa

nguvu zaidi kilimo pamoja na wakulima

kwani faida inayopatikana huwa ni kwa

taifa zima.

Amefahamisha kuwa hali ya Ulimwengu

imebadilika na sisi lazi tubadilike tuwe

na mikakati imara katika kukibadilisha

kilimo chetu kwa faida ya nchi yetu.

Alisema kuwa dhamira ya Wizara ya

Kilimo na Maliasili ndani ya miaka

mitano ni kulima hekta 6,000 za

umwagijiliaji maji, kati ya hekta

8,521 ambapo kwa sasa ni hekta

700 tu ndizo zinazolimwa. Aidha,

alifahamisha kuwa Jamhuri ya Korea

ya Kusini imeahidi kusaidia kulima

hekta 2,000 na Serikali ya Marekani

hekta 2,000.

Aliongeza kusema kuwa mashamba

UPOTEVU WA RUTUBA NA NJIA

ZA KURUTUBISHA ARDHI

Na Hashim H. Chande

Ardhi yenye rutuba ni muhimu

katika ukuwaji wa mimea na

upatikanaji wa mavuno yaliyo bora.

Kama tunavyoelewa kuwa rutuba

ni chakula cha mimea ambacho

kinapatikana kwenye udongo. Ili

kuuweka udongo katika hali ya

rutuba na kuiwezesha mimea

iendelee kukua vizuri ardhini hatuna

budi kutumia mbolea ili kurudisha

chakula kilichochukuliwa na mimea.

Mbolea zinatumika kuongeza

rutuba na kuiwezesha ardhi kutoa

mazao mengi, kinachohitajika ni

jinsi ya kujua aina gani ya mbolea,

kiwango, na wakati zinapohitajika.

Hivyo Mabwana/mabibi shamba

waliomo katika maeneo ya kilimo

wanajukumu la kuwaelimisha

wakulima wa sehemu hizo.

Tishio la upoteaji wa rutuba

darasa yataongezwa hadi kufi kia

1,200, pia mashamba darasa manne

ya mikarafuu yataanzishwa, mawili

Unguja na mawili Pemba.

Mhe. Waziri wa Kilimo aliwaeleza

wakulima kuwa katika bajeti ya Wizara

ya mwaka 2011/2012 itakuwa na

matumaini kwa wakulima wa visiwa

hivi.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja

Mhe. Mustafa Muhammed Ibrahim

aliwatoa hofu wakulima wa bonde

la Kisimamchanga na kuwataka

kuendelea kulitumia bonde hilo kwani

tayari limeshapimwa na Wizara ya

Kilimo kwa lengo la kuanza kilimo cha

umwagiliaji maji.

Nao wakulima wa bonde la

Kisimamchanga wameushukuru mradi

wa PADEP uliotumia zaidi ya shilingi

milioni 32 ambao umeleta mafanikio

makubwa kwa kuongeza uzalishaji

Ardhi iliyopoteza rutuba imeshambuliwa na ukame na hutoa mazao hafi fu au kutoweza

kutoa mazao ya aina yoyote.

4

kutoka polo 4 kwa robo hekta kwa

sasa, wakati hapo zamani walikuwa

wakizalisha polo 4 kwa hekta nzima.

Jumla ya hekta 5 za mbegu ya mpunga

wa aina ya ‘NERICA’ zimevunwa na

zinatarajiwa kupandwa kwa wingi

katika msimu wa mvua za vuli zijazo

kwa lengo la kupandwa wakati wa

masika ambapo zinatarajiwa zaidi ya

tani 3,700 kupatikana katika msimu

ujao wa masika ili kufi kia asilimia 50%

ya uzalishaji ndani ya miaka mitano.

Uzinduzi huo wa kitaifa uliwashirikisha

viongozi kutoka Mikoa 5 ya Unguja

na Pemba, wakiwemo Mawaziri,

Wawakilishi, Mkuu wa Mkoa wa Kusini

ambaye ndiye mwenyeji wa shughuli

hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mjini/

Magharibi, Mkuu wa Mkoa wa Kusini

Pemba, Viongozi wa Serikali pamoja

na Wakisiasa na wananchi kutoka

maeneo mbalimbali.
UPOTEVU WA RUTUBA NA URUTUBISHAJI ARDHI Julai - Septemba, 2011

Mchanganyiko wa vitu tofauti vilivyotumika katika kutengenezea mboji ikiwemo

majani, udongo, takataka, mabaki ya mimea na maji.

katika udongo

Katika nchi yetu tumekabiliwa na

tishio kubwa la kupoteza rutuba

ya udongo kutokana uharibifu wa

mazingira unaosababishwa na

ukataji wa miti ovyo, kuchimba

mchanga, kuchimba na kukata

matofali ya mawe na kilimo

kisichozingatia kanuni bora.

Ardhi inayotumiwa vibaya kwa kilimo

pasi na kurudishia rutuba yake

ni chanzo kikubwa cha upotevu

wa rutuba hiyo ya asili ambayo ni

chakula muhimu cha mimea na

viumbe vyengine vinavyoishi katika

udongo. Upungufu huo husababisha

udongo kupunguza uwezo wake wa

kuhifadhi maji kwa muda mrefu

ambapo ukame hutokea na mazao

yanayopandwa kutoa mavuno

hafi fu.

Rutuba hiyo ni lazima irudishwe

ili tuweze kupata tena mavuno

bora. Hivyo, tunapaswa kuzingatia

urutubishaji wa ardhi kwa kuweka

viwango sahihi vya mbolea

kulingana na mahitaji halisi ya

mimea iliyopandwa, kwa mfano

mpunga unahitaji kiasi cha kilo 100 -

150 cha mbolea kwa kila ekari mbili

na nusu (2.5). Kwa wale wakulima

wenye tabia ya kupumzisha ardhi

kwa kipindi cha mwaka mmoja au

miwili kwa kuchunga wanyama au

kuweka mazizi katika maeneo hayo

wakati wa kupumzisha ardhi, njia hii

husaidia kurudisha rutuba ardhini

ijapokuwa hivi sasa haitumiki sana

katika maeneo mengi kutokana

na ongezeko kubwa la mahitaji ya

ardhi.

Kutokana na ongezeko la mahitaji ya

matumizi ya mbolea za viwandani na

gharama kubwa za upatikanaji wake,

wakulima hatuna budi kujitengezea

mbolea sisi wenyewe kwa kutumia

malighafi tulizonazo kama vile

kupanda mazao ya jamii ya kunde,

matumizi mboji na samadi.

UTENGENEZAJI WA MBOLEA YA

MBOJI

Ili kudumisha uzalishaji wa chakula,

wakulima wa Zanzibar wanasisitizwa

kutengeneza na kutumia mbolea

ya samadi, mboji na takataka pale

ambapo zinapopatikana kwa urahisi.

Mbolea hizi mbali ya kurutubisha

ardhi, pia husaidia kuifanya ardhi

iwe katika hali nzuri iliyoshikamana.

Ingawa wakulima wanahimizwa

kutumia mbolea za viwandani kwa

baadhi ya mazao, lakini sirahisi

kufi dia pengo la mbolea yote

inayohitajika kwa wakati huu ambao

ardhi inaonyesha kuchoka, kutokana

na matumizi mabaya ya mfululizo.

Kupuuza mbolea hizi kunaweza

kuleta madhara makubwa katika

kilimo.

5

Mbolea ya mboji ni mchanganyiko

wa mabaki ya vitu vyenye asili ya

uhai ambavyo hukusanywa kutoka

mashambani na majumbani kama

vile takataka, mabua ya mimea,

magugu, vinyesi vya wanyama au

hata mbolea ya chumvi chumvi.

FAIDA YA MBOLEA YA MBOJI

• Hukaa ardhini na hutumiwa na

mimea kwa muda mrefu, kuliko

mbolea ya chumvi.

• Mboji ina uwezo wa kubadili hali

ya udongo na kuufanya utumike

kwa kilimo.

• Mboji inawezesha udongo

kuhifadhi unyevu kwa muda

mrefu.

• Mboji ni rahisi kutengeneza,

kutumiwa na haina gharama

kubwa ukilinganisha na mbolea

za viwandani.

JINSI YA KUTENGENEZA

i Safi sha eneo unalotaka

kutengeneza mbolea.

ii Pima mita 1.5 urefu na mita 1.5

upana na weka fi to baada ya

kupima urefu na upana, urefu

wa fi to unategemea mahitaji ya

mkulima.

iii Chimbua chimbua na weka vizuri

udongo.

iv Panga tabaka la udongo, majani,

mabua na kuyatandaza pamoja

na takataka zinazoweza kuoza.

iii Weka tabaka la udongo wa

kutosha juu mabua na majani

kwa mpangilio.

iv Tumia mbolea ya chumvi chumvi

au vinyesi vya wanyama kwa

kunyunyizia juu ya udongo.

v Nyunyizia maji baada ya kuweka

mbolea, kwa kumalizia tabaka la

kwanza. Rudia kuweka tabaka la

pili mpaka la tatu juu yake kwa

kufata mpangilio ule ule wa

tabaka la mwanzo hadi kufi kia

urefu wa mita 1-2.

vi Hakikisha tabaka lina unyevu na

joto la kutosha. Geuza tabaka

hizo kila baada ya wiki mbili

kwa kupunguza hewa na unyevu

uliozidi ili kuozesha takataka

kikalifu.

vii Mbolea hiyo inatakiwa itumike

baada ya kuoza na kupoa.
Julai - Septemba, 2011 KARAFUU

UVUNAJI NA UANIKAJI KARAFUU

Na Rashid Khamis

Zanzibar imekuwa ikijulikana

sana katika uuzaji wa karafuu

bora kuanzia karne ya 18, karafuu

bora zinapatikana kutoana na

uchumaji, uchambuaji, uanikaji

bora pamoja na usafi shaji wa

karafuu kabla ya kuuza. Katika

miaka ya 2000 tumeshuhudia

kurejeshwa kwa uchafu wa

karafuu zilizouzwa nje katika

Shirika la Biashara la Taifa

la Zanzibar (ZSTC) Hali hii

inasababisha Zanzibar kupoteza

sifa yake ya kuuza karafuu bora.

UVUNAJI

Karafuu nzuri kwa biashara

ni yenye rangi kutoka kijani

na kuingia rangi ya manjano

kabla ya kuchanua. Karafuu

ikachanua inabadilika na kuwa

mbegu na hupoteza matumizi

yaliyokusudiwa.

Wakati wa uchumaji wa karafuu ni

vizuri kuepuka ukataji wa matawi

kwani tabia hii hudhoofi sha

mikarafuu na husababisha

kushambuliwa na maradhi na

hatimae kufa.

Mwananchi akiwa katika harakati za kuvuna karafuu ili kuliokoa zao hili

la kitaifa lisipotee

Wakati wa kuchuma, matawi

dhaifu ya mikarafuu mikubwa

yafungwe pamoja kwa kutumia

kamba. Aidha Hii itasaidia

kufanya yawe madhubuti zaidi,

hivyo kupunguza uwezekano wa

kukwanyuka kutokana na uzito

wa mchumaji. Kamba au vingoe

Mwanamama akiwa mstari wa mbele katika kushiriki kuchambua

karafuu kwa lengo la kuliokoa zao hili la Taifa

6

vitumike kwa kuvuta matawi

yaliyombali ili yaweze kuchumwa

kirahisi badala ya kuyavunja.

Mikarafuu midogo inaweza

kuchumwa kwa kutumia ngazi na

hii inasaidia kupunguza kwa kiasi

kikubwa uharibifu huo.

UANIKAJI

Karafuu zianikwe haraka baada

ya kuchambuliwa na kusafi shwa

na hakikisha sehemu za kuanikia

zinapata jua wakati wote (kutwa

nzima). Usianike karafuu karibu

na jengo lolote au miti mirefu

inayoweza kutoa kivuli.

Miongoni mwa vifaa vilivyo bora

kwa kuanikia karafuu ni majamvi

kwa sababu huhifadhi karafuu

vizuri zaidi wakati wa mvua

kuliko aina nyengine za vifaa

kama magunia. Magunia yakiroa

hufyonza maji na kurowesha

karafuu, pia hupunguza gredi

kwa kutoa nyuzi ambazo

huchanganyika na karafuu.

Karafuu zinazoanikwa juu ya

sakafu ziendelee kuwekwa kwenye

majamvi kwa vile sakafu huchuna
KARAFUU Julai - Septemba, 2011

karafuu wakati wa kugeuza na

kuanua. Inashauria majamvi

yawekwe juu ya majani mafupi

kuepuka kuingia vumbi. Haitakiwi

kuanika karafuu pembezoni mwa

barabara ili kuepusha kupoteza

ubora wake kwa kuchanganyika

na vitu vengine, kupondwa na gari

au kukanyagwa na wapita njia.

Karafuu bora zinatakiwa ziwe na

sifa zifuatazo:

• Ziwe hazina vitawi, vijiti na

matende nzima na zenye

umbo la namna moja

zisizoganda, hazina makonyo,

mabegu, mpeta na takataka

nyenginezo. Ziwe kavu kwa

kiwango cha kukatika vipande

viwili kwa kutumia vidole na

zenye rangi ya zafarani.

Karafuu zina madini ya Calcium,

Iron, Phosphorus, Sodium,

Potassium, Hydrochloric acid,

na vitamin A na C. Historia

inatwambia kuwa katika karne

ya tatu B.C, China iliweka sheria

kuwa kabla ya kuzunguza na

mfalme lazima kusafi sha mdomo

kwa kutumia karafuu. Aidha zaidi

ya miaka 2000 iliyopita Wachina

na Wahindi walizitumia karafuu

kama viungo katika vyakula,

dawa ya magonjwa ya meno

na kuondosha harufu mbaya ya

kinywa.

MATUMIZI YA KARAFUU

Madawa

Karafuu ina nguvu za kuponyesha

magonjwa kama ifuatavyo:

• Mafuta ya karafuu yanatumika

katika kuponyesha maumivu

ya meno, vidonda vya ufi zi na

mdomo, hali hii imepelekea

kuingizwa katika dawa za

msuwaki na za kusukutuwa.

Zinc huchanganywa na mafuta

ya karafuu kwa kutibu meno

yenye pango.

`• Mafuta ya karafuu yakipakwa

katika kidonda au mchubuko

huzuwia maradhi ya “fungus”

pia hupunguza maumivu

baada ya kupaka sehemu

ambayo umetafunwa na

wadudu. Ngozi iliyopakwa

mafuta ya karafuu huwa

nyororo na huhifadhika na

magonjwa. Hata hivyo, mafuta

ya karafuu ni makali sana na

yanahitaji kuzimuliwa.

• Mafuta ya karafuu

yanachangamsha na

kuondoa uchovu wa akili na

mwili, upatikanaji usingizi

ikiwa utakunywa kidogo pia

hutumiwa katika kufanya

masaji ambayo huondoa

uchofu wa mwili.

• Mafuta ya karafuu

yakichanganywa na chumvi na

kupakwa kikomoni huondosha

maumivu ya kichwa. Karafuu

zikitafunwa husaidia kusafi sha

koo, kuponya kifua na pumu.

• Mchanganyiko wa mafuta

ya karafuu na mafuta ya

ufuta yakipakwa katika ngozi

huponya magonjwa ya upele.

• Mafuta ya karafuu yanasaidia

kusafi sha damu, kuengeza

7

mzunguko wa damu na

kuengeza kinga ya mwiili.

• Mafuta na karafuu zinatibu

maradhi ya tumbo.

Vipodozi, sabuni na mafuta

mazuri.

• Mafuta ya karafuu (creams )

na mafuta ya kupaka (lotions)

hulainisha ngozi na kuwa

nyororo.

• Mafuta ya karafuu pia

yanatumika katika

kutengeneza mafuta mazuri.

Sigara

Karafuu zinachanganywa na

tumbaku na kutengenezwa sigara

zenye ladha nzuri ya karafuu.

Chakula

Karafuu inatumika kuongeza

ladha katika vyakula kama pilau,

uji, keki, “pudding” na “sausage”.

Unga wa karafuu unachanganjwa

pamoja na unga wa viungo

vyengine kutengeneza masala.

Karafuu zinahitaji kuanikwa katika maeneo yaliyosafi ili kuepuka

kuchanganyika na takataka kwa lengo la kupata gredi iliyo bora
Julai - Septemba, 2011 MATUKIO KA

Matukio ka

Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Mohamed Ali Shein

akitia saini katika kitabu cha wageni baada ya kuzinduwa uvunaji wa mbegu ya mpunga aina

ya NERICA katika Kituo cha Uzalishaji wa mbegu, Bambi.

Wakulima hujifunza zaidi mbinu bora za uzalishaji wa mazao wanapopata fursa za kushiriki

katika ziara za kimafunzo ambapo hupata wasaa wa kudadisi pamoja na kubadilishana

uzoefu walionao wao wenyewe katika kuendeleza kilimo.

8

Wakulima wa mpunga wa bonde la Mtwango n

ya zana za kisasa ikiwemo matrekta madogo

uburugaji wa mashamba ya mpunga.

Upandaji wa mikoko katika maeneo ya pwani

mazingira ya pwani yaliyoharibiwa kutokana n

tatizo la kuharibika fukwe na kupanda maji katik
TIKA PICHA Julai - Septemba, 2011

tika Picha

a Bumbwisudi wako mbele katika matumizi

(Power tiller) katika kazi za uchimbuaji na

ni njia moja wapo ya kutunza na kudhibiti

a ukataji ovyo wa mikoko ili kukabiliana na

a maeneo ya kilimo..

Wafanyakazi wa Kitengo cha Utibabu wa Mimea wakiwa katika kazi za kuweka dawa ya

kunasia nzi wa matunda katika mitego maalum ili kukabiliana na tatizo hilo ambalo linarudisha

nyuma juhudi na maendeleo ya wakulima katika kukuza zao la matunda.

Wizara ya Kilimo na Maliasili katika juhudi zake za kukuza kilimo cha umwagiliaji maji inaendelea

kujenga miundombinu ya umwagiliaji maji kama ilivyoainishwa katika Mpango Mkuu wa Taifa wa

Kilimo cha Umwagiliaji maji kwa lengo la kwawezesha wakulima kuongeza uzalishaji na tija.

9
Julai - Septemba, 2011 MABARAZA YA WAKULIMA

MABARAZA YA WAKULIMA NI CHACHU YA

MAENDELEO YA KILIMO ZANZIBAR

Na Shauri Haji

Mabaraza ya wakulima (Farmers

Fora) yaliyoanzishwa miaka minne

iliyopita katika wilaya tisa za Unguja na

Pemba na Programu za Kuimarisha

Huduma za Kilimo na Maendeleo ya

Mifugo (ASSP na ASDP-L) Zanzibar ni

vyombo muhimu vya kuwaunganisha

wakulima ingawa dhana hii ni ngeni

katika visiwa hivi.

Mabaraza hayo ya wakulima

yameanzishwa katika Wilaya ya

Magharibi, Kati, Kusini, Kaskazini A na

Kaskazini B, kwa upande wa Unguja na

Wilaya ya Mkoani, Chake chake, Wete

na Micheweni kwa Pemba.

Mabaraza hayo licha ya kuwa na

changangamoto za kiutendaji tangu

yaanzishwe, yamekuwa ni chachu

kwa maendeleo ya kilimo na mifugo

sambamba na kuwa na sauti ya

kumtetea mkulima. Hata hivyo, bado

kuna dhana kwamba programu za

ASSP na ASDP-L ndizo zenye jukumu la

kugharamia ma baraza hayo.

Dhana ya kuanzishwa kwa Mabaraza ya

Wakulima imekuja baada ya kuona ipo

haja kwa wakulima kuwa na chombo

chao cha kuwaunganisha ili waweze

kutatua matatizo yao kwa pamoja,

kuzijua haki zao na kuzitetea. Tangu

kuanzishwa kwa mabaraza hayo

wakulima wameweza kutatua migogoro

yao ya ardhi hasa katika maeneo yaliyo

nje ya utekelezaji wa miradi ya ASSP na

ASDP-L.

Katibu wa Baraza la wakulima la

Wilaya ya Kati Unguja Bi Mashavu

Juma Mapuri ambae pia ni katibu

wa skuli ya wakulima (FFS) ya Mwera

Kichaka Mabuzi, alisema kwamba

wakulima katika shehia mbali mbali

wanaamini kuwa hiki ni chombo pekee

kinachotumika kupata taarifa na ushauri

kuhusu maendeleo ya uzalishaji wa

mazao ya kilimo na mifugo, kuwatetea,

kuwasemea na kushawishi kuhusu

haki zao na kuwa na sauti ya pamoja ya

kufi kisha maoni na matatizo yao bila

woga kwa wahusika.

Alifahamisha juhudi kubwa zilichukuliwa

kuwashajiisha wakulima kutoka shehia

nyengine kujiunga na chombo hicho

na kuondoa dhana potofu miongoni

mwa wakulima kwamba Mabaraza hayo

ni kwa ajili ya shehia zinazotekeleza

miradi iliyo chini ya programu za ASSP

na ASDP-L na kwamba wakulima wa

Waziri wa Kilimo na Maliasili Mhe. Mansor Yussuf Himid aliyesimama akiwa

anasisitiza mshikamano wa wakulima wakati akizungumza na wajumbe wa

Mabaraza ya Wakulima huko Dunga Wilaya ya Kati, Unguja.

shehia nyengine hawahusiki. Hali

hiyo imewajengea imani wakulima na

kuweza kufuatilia kwa karibu taarifa

katika Mabaraza ya Wakulima.

Mabaraza hayo yaliundwa kwa

lengo la kujenga mashirikiano ya

karibu na watoa huduma binafsi na

kuwajengea uwezo wakulima kitaaluma

na kuwawezesha kuongeza uzalishaji

wenye tija na kupunguza umasikini na

kuongeza kipato. Mabaraza haya kwa

kawaida huwa na wanachama 20

akiwemo Mwenyekiti, Katibu na Mshika

fedha pamoja na wajumbe 17 kwa kila

baraza la Wilaya.

Miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana

ni pamoja na kuwatembeza wakulima

50 wa muhogo na mazao mengine

katika kikundi cha “Nguvu Kazi

Tusizembee” cha Kisongoni wilaya ya

Kaskazini ‘A’ kinachojishughulisha na

ukulima wa mpunga ambapo wakulima

hao walipata maelezo, kuhamasika

na kuanzisha kilimo cha mpunga

katika maeneo yao. Hayo yalielezwa

na Mwenyekiti wa Baraza la Wakulima

la Wilaya ya Kaskazini A nd. Abeid Ussi

Haji.

Waziri wa Kilimo na Maliasili,

Zanzibar Mhe, Mansoor Yussuf Himid

10

akizungumza na Baraza la Wakulima

la Wilaya ya Kati, Dunga amekuwa

na imani kubwa na Mabaraza hayo

yaliyoanzishwa Unguja na Pemba.

Aidha, aliwaeleza wakulima Serikali ya

awamu ya saba inayoongozwa na Mhe.

Dk. Ali Mohamed Shein imekusudia

kuleta mageuzi makubwa katika kilimo

kwa kupunguza gharama za pembejeo

muhimu kwa asilimia 75% zikiwemo

mbolea, mbegu, madawa, gharama za

kuchimba na kuburuga ili kumwezesha

mkulima kumudu gharama hizo.

Waziri amelihakikishia baraza la

wakulima kwamba Wizara yake

inakusudia kuimarisha miundombinu

ya masoko, kuongeza thamani ya

mazao ya kilimo na kujenga barabara

ndogo zinazoingia mashambani kwa

kuziunganisha na barabara kuu ili

kurahisisha usafi rishaji wa mazao ya

wakulima.

Aidha, aliwahakikishia wakulima kuwa

mbegu mpya ya mpunga aina ya

NERICA inayoota katika maeneo ya

juu itazalishwa na kusambazwa kwao

ili waweze kuzalisha zaidi. Wastani

wa tani 140 za NERICA zinatarajiwa

kuzalishwa ili kila mkulima aweze

kutumia mbegu bora kutoka asilimia

zero hadi kufi ka asilimia 33.6.
ATHARI YA JOTO Julai - Septemba, 2011

ATHARI YA JOTO KWA MIFUGO

Na Nassor S. Mohammed

Hali ya hewa inajumuisha ujoto,

unyevu wa hewa, mvua, upepo,

miale ya jua, uzito wa hewa pamoja

na mazingira yote katika maeneo

husika. Kwa kawaida hali ya ujoto

na mvua huwezesha mimea na

mifugo kuishi na kukua vizuri.

Mifugo ni miongoni mwa viumbe

ambavyo hutegemea sana

hali ya hewa katika kuishi na

kuzalisha mazao kama maziwa,

nyama, mayai, manyoya na ngozi

ambavyo hutumiwa kwa chakula,

kutengeneza makoti ya baridi,

mikanda, mikoba na masofa.

Wanyama hawa wanahitaji

hali ya hewa ambayo ni nzuri

kwa ajili ya kuishi na kuzalisha

pindi ikikosekana athari zake

hujitokeza.

Kwa kawaida wanyama wakubwa

wanahitaji joto lenye nyuzi joto kati

ya 37 - 40 sentigredi na wadogo

wanahitaji joto la mwili kati ya nyuzi

joto 40- 44 sentigredi, mfano:

Ng’ombe...............38.5 0 C

Kondoo.................38.0 0 C– 39.5 0 C

Kuku wa mayai wanahitaji joto la wastani ili waweze kula na kunywa maji kwa

wingi, hali ambayo huchangia zaidi katika utagaji wa mayai.

Mbuzi....................40 0 C

Farasi....................38 0 C

Mbwa....................39 0 C

Paka......................38.5 0 C

Sungura................39.3 0 C

Kuku......................42.1 0 C

Bata.......................21 0 C

Mifugo kama ng’ombe hukuwa vizuri zaidi na kutoa maziwa kwa wingi ikiwa

itawekwa katika maeneo ambayo yana kivuli na kupitisha hewa ya kutosha.

11

Mifugo inapokuwa na joto jingi

katika miili yao, mara nyingi hutoa

jasho na mwili hupoteza joto hilo na

akihisi baridi huzuia utoaji wa jasho

na ujoto hubaki mwilini.

Malisho

Hali ya hewa huchangia katika

uimarikaji wa malisho, ulaji na

ukuaji wa mifugo. Mifugo kama

ng’ombe, mbuzi na kondoo

wanapokuwa machungani

ikiwa hali ya hewa ni ya joto kali

hushindwa kutembea na kujitafutia

chakula pia malisho huwa hafi fu.

Hivyo mifugo hukosa chakula cha

kutosha na kushiba. Ng’ombe wa

kienyeji wanaweza kustahamili hali

ya joto ukilinganisha na ng’ombe

wa makabila ya nchi za baridi au

machotara.

Hali ya ubaridi huimarisha malisho

na huiwezesha mifugo kutumia

muda mwingi machungani kujipatia

chakula zaidi badala ya kukaa

kivulini. Ng’ombe na mbuzi wa

kabila za kigeni, mfano Friesian,
Julai - Septemba, 2011 ATHARI ZA JOTO

Jersey na Saanen, Norwegian na

machotara huhitaji chakula kingi

zaidi wakikosa huathirika.

Katika nchi za joto kuna vipindi vya

mvua nyingi ambapo mimea hukua

haraka na kupea mara moja. Kwa

kawaida mifugo hula kidogo sana

majani yaliyokomaa hata kama

itakuwa na njaa kwa sababu majani

hayo yana desturi ya kutoa joto jingi

yanaposagwa mwilini hivyo, joto

jingi husababisha mifugo kutoweza

kula vizuri chakula hicho kwa

manufaa ya miili yao na uzalishaji.

Vyakula vya ziada

Mbali na majani, vyakula

vyengine vya ziada kama vile

mabaki ya vyakula vilivyoliwa na

binadamu, maganda ya muhogo,

viazi, magomba, masalia ya

mashambani, pumba, mashudu

na madini yanahitajika kulishia

wanyama. Vyakula hivi ambavyo

hupunguza na havitoi joto jingi

mwilini ni vizuri kupewa wanyama

hasa mifugo ya kabila za nchi za

baridi na machotara ambao kwa

kawaida wanahitaji chakula kingi.

Vyakula vya mifugo vinatakiwa

viweze kupoza joto la mwili yaani

vyenye protini. Ng’ombe huacha

kula kabisa wakati mwili wake

ukiwa na joto kali.

Maji

Maji ni muhimu sana katika ukuaji

na uzalishaji wa mifugo na mazao

yake hivyo mifugo inahitaji maji kwa

sababu kuu mbili:

Maji ni chakula na ni sehemu ya

mwili wao. Maji hupoza joto la mwili

linalotokana na usagaji na matumizi

ya chakula katika kiwiliwili.

Joto linafanya mifugo inywe maji

mengi, kwa ng’ombe wa kigeni wa

maziwa mwili ufi kapo nyuzi joto

29.4 sentigredi unywaji wa maji

hupungua na kusababisha ulaji wa

chakula kuwa mdogo hivyo kuathiri

uzalishaji.

Mifugo iliyozoea maeneo na

mazingira yake hunywa maji kidogo

ukilinganisha na ile ambayo ni

wageni katika eneo hilo mfano

kutoka kwenye baridi kuja kwenye

joto na mvuke mwingi hewani

huifanya mifugo inywe maji mara

kwa mara.

Utoaji wa maziwa

Joto kali husababisha uzalishaji wa

maziwa kuwa mdogo na kuharibika

kirahisi. Ng’ombe wa kigeni

kama Jersey na Friesian wanatoa

maziwa mengi katika mazingira ya

baridi lakini joto likizidi njuzijoto

10 sentigredi ng’ombe hawa

hupunguza maziwa na ifi kapo

nyuzijoto 21 hadi 27 sentigredi,

utoaji wa maziwa hushuka kwa

kiwango kikubwa.

Uzazi

Joto, unyevu wa hewani na

mwangaza unachangia katika

kiwango cha uzalishaji wa mifugo.

Joto jingi mwilini linaharibu

mbegu za uzazi za kike na za

kiume pamoja na mayai ambayo

yamepandishiwa yakiwemo katika

harakati za kufanya mtoto. Vizazi

12

vinavyozaliwa nyakati za joto kali

na kutohifadhiwa katika mazingira

mazuri hufa kwa urahisi. Aidha,

joto kali linapunguza utagaji wa

mayai kwa jamii ya kuku.

Maradhi

Hali ya joto inachangia kuishi,

kukua na kuzalisha vimelea na

viumbe vinavyosababisha maradhi

kwa mifugo. Mifugo ya makabila

ya kigeni huathiriwa kirahisi na

kupata maradhi. Mazingira mazuri,

shibe na maji husababisha mifugo

kukua haraka, kuwa na afya nzuri

na kuweza kuhimili maradhi.

Mazao ya mifugo

Mazao mengi ya mifugo, mfano

maziwa, nyama na mayai huharibika

haraka yakiwekwa katika hali

ya joto. Ndugu wafugaji inafaa

kuchukua tahadhari ya kutunza

mazao hayo katika maeneo yenye

baridi, pia tunaombwa tutayarishe

malisho kwa ajili ya wakati wa

kiangazi ili wanyama wetu wapate

malisho bora na kuongeza

uzalishaji.

Mbuzi wa maziwa pia wanahitaji mabanda yaliyoinuka, yenye kupitisha hewa na

mwanga wa kutosha ili waweze kukua vizuri na kutoa maziwa kwa wingi.
UJASIRIAMALI Julai - Septemba, 2011

MBINU BORA ZA UJASIRIAMALI

Na Haji A. Omar

Ujasiriamali ni uwezo wa kumudu

na kuendesha biashara kwa

faida katika mazingira ya ushindani

sokoni, uhaba wa mtaji na bila ya

kujali hasara nyengine.

Mjasiriamali ni nani?

Ni mtu ambaye ana maono

ya biashara, mwenye uwezo

wa kugundua fursa, mwenye

msukumo wa kukusanya rasilimali

na kuthubutu kuanzisha mradi kwa

imani kwamba atafanikiwa katika

biashara yake.

Sifa kuu za Mjasiriamali:

• Mwenye kutafuta fursa

• Anaetimiza makubaliano

katika biashara

• Mwenye utashi wa ubora na

ufanisi katika kazi yake

• Mwenye malengo ya muda

mfupi na muda mrefu

• Mwenye uwezo wa kupanga

na kusimamia kazi yake

• Mwenye ari ya kutafuta

habari

• Mwenye uwezo wa

kushawishi na kutoa

ushirikiano

• Anaejiamini na kutenda

Ijapokuwa watu wengi husema

kwamba uwezo wa kijasiriamali ni

kipaji cha kuzaliwa na huthubutu

kufananisha na baadhi ya makabila

yanayofanikiwa kibiashara kama

vile, Wakikuyu-Kenya, Wahindi na

Waarabu-Asia, Wachaga-Tanzania

Bara na Wapemba-Zanzibar. Watu

wengine husema Ujasiriamali

unapatikana kwa kusomea, Je nani

yuko sahihi kati ya wenye hoja mbili

hizi?

Utafi ti uliofanywa sehemu tofauti

duniani haukubaliani na hoja ya

kwanza pekee, kuwa mjasiriamali

hamilikiwi na kundi fulani pekee

Mjasiriamali anaweza kuekeza katika biashara yoyote ile bila ya kujali kutokea kwa

hasara, kinu cha kusagia nafaka ni moja ya biashara hizo.

katika jamii bali mjasiriamali

anaweza kutoka katika kabila

na jamii yoyote duniani. Vile vile

watalamu wengi wanakubaliana

kwamba Mjasiriamali akiwa na

sifa zote mbili ndio muamala zaidi

kuliko kuwa na kipaji cha kuzaliwa

pekee.

Kila mtu anaweza kuwa mjasiriamali,

cha muhimu ni kuamua, kujituma

na kutenda. Baadhi ya wataalamu

wanasema hakuna mtu anaezaliwa

mjasiriamali, bali watu wengi huiga

au kujifunza ujasiriamali kutoka

kwa waliowazunguka kama vile

wazazi, walezi au kupitia mafunzo

ya fani hiyo. Kwa mantiki hiyo,

yeyote anaweza kuwa mjasiriamali

na mwenye mafanikio makubwa ya

kupigiwa mfano.

USIMAMIZI NA UENDESHAJI WA

BIASHARA ZA KILIMO

Biashara za kilimo

Zinajumuisha utaratibu mzima wa

kupangilia matumizi ya pembejeo

za kilimo ili kuweza kudhibiti na

kutambua uhusiano baina ya

13

pembejeo zilizotumika na mazao

yaliyopatikana katika kipindi

cha uzalishaji. Utaratibu huu

unahusiana na kuelewa uchumi

wa kilimo na mbinu za ujasiriamali

katika kumudu na kuendesha

miradi midogo na mikubwa.

Usimamizi na uendeshaji

Ni utendaji wa kazi kwa kutumia

mtu au kikundi cha watu pamoja

na rasilimali nyingine kwa utaratibu

maalum uliopangwa ili kuweza

kufi kia malengo yaliyokusudiwa.

Kazi za usimamizi na uendeshaji

ni pamoja na kupanga, kuongoza,

kuhamasisha, kuajiri, kudhibiti na

kutathmini.

Mambo muhimu ili msimamizi

aweze kufanya kazi zake vizuri:

• Awe mwenye kuielewa kazi

yake vizuri

• Atoe au kupata motisha

• Afuate taratibu za sheria

• Awe mwenye kufahamu

mazingira ya kazi

• Awe na uwezo wa kufanya
Julai - Septemba, 2011 UJASIRIAMALI

tathmini ya kazi

Sifa za mjasiriamali katika

kusimamia biashara:

1. Kuweka malengo kwa

usahihi na yawe mahsusi,

yanayopimika, yanayofi kika,

yanayofaa na yanayoweza

kufuatiliwa.

2. Kuwa na mfumo wa taarifa na

kuweka kumbukumbu kama

vile kudhibiti na kutathmini

maendeleo, kufanya maamuzi

na kupanga mipango ijayo,

kuelewa mbinu mpya juu

ya teknolojia, masoko na

mazingira.

3. Muda ni bidhaa muhimu kuliko

bidhaa nyengine na kama

muda hautunzwi hakutakua

na maendeleo mazuri. Muda

ni kigezo kikuu cha utendaji

ukitunzwa huleta ufanisi.

Kutunza muda ni kugawa muda

huo kwa ajili ya kuweka malengo

kwa umuhimu wake, kugundua

na kuondosha vipoteza muda na

kutumia maarifa ya uongozi ili

kufi kia malengo kiufanisi zaidi.

Mambo ya kuzingatia:

• Hakuna namna ya kuweza

kufi dia muda – Dakika

moja iliyopotea haiwezi

kurudi tena

• Panga mambo yako kwa

vipaumbele ili kuokoa

muda

• Hakuna muda mchache,

kuona muda mchache ni

dalili za uongozi mbaya

• Kulala wakati wa usiku ni

njia pekee ya kupumzika na

sio kucheza gemu au kukaa

maskani wakati wa mchana

kama ndio njia muafaka ya

kupumzika

Mambo yafuatayo husababisha mtu

kupoteza muda bila kujijua au kwa

kujua kwa maana ya kupumzika:

• Kucheza gemu na kuandika

ujumbe wa maandishi sana

katika simu

• Kupokea na kufurahia

wageni wanaokuja bila

miadi

• Kutoweka malengo na

vipaumbele vya kazi

• Kucheza karata, draft na

bao la kete wakati wa kazi

• Dawati lililojaa karatasi bila

mpango

• Kutogawa kazi kikamilifu

au kufanya kazi zinazoweza

kufanywa na walio chini

yako

• Kufanya mambo mengi kwa

wakati mmoja

• Kushindwa kusema hapana

au siwezi

• Ukosefu wa nidhamu

4. Motisha ni kitu chochote

kinachohimiza juhudi katika

kazi. Kwa kawaida binaadamu

akipata motisha huongeza

juhudi. Vifuatavyo ni vitu

vitolewavyo ili kuongeza juhudi:

• Motisha kwa wafanyakazi

ni kama vile kumpandisha

cheo, kupata bonasi

yanapotokea mafanikio

makubwa na ongezeko la

mshahara

• Motisha kwa wateja ni

kama vile kupunguza bei,

usafi ri wa bure, nyongeza

ya kitu juu ya bidhaa

aliyonunua, huduma

nzuri kwa mteja ukiwemo

14

ukarimu na uchangamfu.

5. Mawasiliano kwa mjasiriamali

ni njia pekee ya kupokea

habari kwa haraka, husaidia

wateja kuelewa huduma,

biashara au bidhaa zitolewazo

na kupokea maoni ya wateja.

Usipoitangaza biashara yako na

kutafuta taarifa itakua vigumu

kuingia katika ulimwengu wa

biashara, kama vile usemi

maarufu usemavyo “BIASHARA

ITANGAZWAYO NDIO ITOKAYO”

Zipo njia tofauti za mawasiliano

zinazotumiwa na wajasiriamali.

Miongoni mwake ni :

• Mawasiliano kwa

maandishi kama vile

mabango ya matangazo,

barua, vipeperushi, ripoti,

lebo za kwenye bidhaa

humuwezesha mjasiriamali

kuwasiliana na wateja

wake au wadau wengine

wa biashara.

• Mawasiliano kwa njia ya

maongezi kupitia mijadala,

warsha, kongamano,

semina na mikutano.

Mjasiriamali anaweza

kupata muda mzuri wa

kuwasiliana na wateja kwa

kushiriki kwenye mafunzo

ya shamba darasa, sehemu

za maonyesho ya bidhaa

kama vile maonesho ya

biashara na ya wakulima

• Mawasiliano ya ishara kama

vile ishara za uso, mikono,

mabega na kichwa, njia

hii hutumika kwa wateja

au wadau wengine wa

biashara mara nyingi njia

hii hutoa ujumbe mzuri au

mbaya. Hivyo mjasiriamali

lazima awe makini na

ishara atoazo mteja hata

kama wateja wanawasiliana

wao wenyewe wanapokuwa

katika eneo la biashara.
RASILIMALI ZA MSITUNI Julai - Septemba, 2011

UMUHIMU WA RASILIMALI ZA MSITUNI

Na Nassor S. Mkarafuu

Rasilimali za msituni zina uasili

wa kibaiolojia zikijumuisha

wanyama na mimea ya aina na

rika tofauti yenye faida kwa maisha

ya viumbe pamoja na huduma

zinazopatikana msituni au ardhi

inayotumika. Kuwepo kwa rasilimali

hizi kunategemea uwepo wa msitu.

Rasilimali za msituni zina faida

nyingi kwa maisha ya viumbe

wakiwemo binadamu, wanyama

na wadudu. Miongoni mwa faida

za moja kwa moja ni upatikanaji

wa chakula, miti ya mapambo,

vichanganyisho vya manukato,

mbegu pamoja na upatikanaji wa

wanyama na mimea yenye kutoa

tiba.

Faida nyengine ni pamoja na

uhifadhi wa vyanzo vya maji,

kurekebisha hali ya hewa, ufyonzaji

wa hewa mkaa, uhifadhi wa udongo

na kuzuia mmong’onyoko, ambapo

katika nchi nyingi za Afrika,

rasilimali hizi zina umuhimu wa

upatikanaji wa lishe kwa kaya.

UTEGEMEZI WA JAMII KWA

MAZAO YAPATIKANAYO MSITUNI

Duniani kote jamii zinategemea

rasilimali zinazopatikana msituni

ikiwemo kujikimu kwa chakula,

malisho ya wanyama, madawa na

zana za ujenzi. Matumizi mengine

ni pamoja na kupatikana zana

za ukulima, utengenezaji wa

mapambo ya majumbani.

Nchi nyingi za Afrika na Asia,

jamii hutegemea rasilimali hizo

kwa kuongeza kipato cha kaya,

kupata uhakika wa chakula na

lishe, biashara na ajira kwa

ujumla. Hata hivyo rasilimali hizo

hazipewi umuhimu na wanasiasa

na wapangaji wa mipango ya

Maendeleo licha ya umuhimu wake,

mara nyingi watu hutoa thamani

ya msitu pale tu yanapopatikana

mavuno yake, kuyatumia,

kutengeneza bidhaa, kuziuza na

kuchangia kuoengeza kipato kwa

jamii za vijijini. Rasilimali hizi ni

kiashirio kikubwa katika kupunguza

Misitu huchangia katika upatikanaji wa rasilimali nyingi pamoja na umuhimu

wake husaidia katika kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji.

umasikini kwa jamii zinazotegemea

msitu kwa kuongeza kipato, kupata

uhakika wa chakula.

Uhakika wa Chakula na Lishe

Rasilimali za msituni zina mchango

mkubwa katika kuchangia uhakika

wa chakula na lishe katika jamii

kwa nyanja tofauti kama vile

kupata chakula kinachochangia

kutoa vitamini, madini, uanga

na protini muhimu. Jamii nyingi

za vijjini zinatumia vyakula

vinavyopatikana msituni kwa kula

au kuuza kwa lengo la kupata pesa

za kununulia chakula hasa wakati

wa uhaba wa mavuno ya mazao

mashambani. Miongoni mwa

mazao yanayopatikana msituni

ni pamoja na matunda, mboga

mboga, wanyama pori na asali.

Matunda

Mabungo, Zambarau, Fuu, Ukwaju,

Ubuyu, Mapera, Pilipilidoria, Maviru,

Kunazi na Chongoma. Aidha, katika

baadhi ya nchi za Afrika mazao

kama edible nuts zinatumika kwa

chakula, mafuta ya kula, viungo,

achari na vinywaji.

Mbogamboga

15

Miongoni mwa mboga

zinazopatikana ni kikwayakwaya,

pwipwi, mchicha mwiba, mchunga,

mronge, mchambale, mboga ya

pwani na mnavu. Aina hizi za mboga

za asili zinatoa madini mengi zaidi

kuliko aina ya mboga zisizokuwa za

asili. Inasemekana mboga za asili

zina madini ya chokaa (calcium)

1.5 – 3.2 zaidi ya mboga mboga za

jamii ya kabeji ambazo ndizo zenye

madini ya chokaa (calcium) nyingi

kwa mboga zisizokuwa za asili.

Wanyama pori

Wanyama pori ni miongoni mwa

chakula muhimu katika kuongeza

uhakika wa chakula na lishe

wakijumuisha wanyama, ndege

na mayai yao pamoja na samaki.

Nyama itokanayo na wanyama

hawa ni chanzo cha protini na

madini mengine kama chuma,

vitamin A na B. Wanyama wadogo

(paa) na ndege (kanga) ni maarufu

katika kuongeza chakula na lishe

ya jamii.

Asali

Ni miongoni mwa chakula maarufu

hapa nchini. Kawaida asali iliyo

nyingi hutengenezwa na nyuki

na hupatikana msituni baada ya
Toleo la Saba

Julai - Septemba, 2011

kuvunwa ambayo hutumika katika

jamii kwa kula, dawa na biashara.

miongoni na Faida nyengine,

masega ya nyuki hutumika katika

kutengeneza mshumaa na maji

maji yaitwayo royal jelly.

Matumizi ya asali yanatofautiana

kutoka sehemu moja hadi nyengine

kutokana na upatikanaji na hali

ya soko. Wananchi wa vijijini mara

nyingi hutumia asali kama dawa ya

kutibu maradhi mbali mbali pamoja

na kuuza kwa kujiongezea kipato.

Hapa Zanzibar lita moja inauzwa

kwa wastani wa shilingi 12, 000.

Hii inamaanisha kwamba asali

ni moja kati ya rasilimali yenye

umuhimu katika afya na kuongeza

kipato katika jamii.

Dawa za asili

Dawa za asili ni mazao muhimu

yanayopatikana kutoka msituni

ambapo nchi zote za Afrika

zinatumika. Zaidi ya watu bilioni

3.5 wanaoishi pembezoni mwa

misitu duniani wanatumia dawa

za asili na inakisiwa aina 35,000

zinatumika ambapo katika nchi

za Afrika zaidi ya asilimia 80 ya

watu wanatumia dawa za asili kwa

matibabu ya maradhi na maumivu

mbali mbali. Shirika la Afya Duniani

(WHO) limekisia kwamba zaidi ya

asilimia 80 ya watu katika nchi

zinazoendelea wanategemea dawa

za asili kwa matibabu ya msingi na

zinapatikana kwa urahisi na jamii

inazifahamu.

Miongoni mwa miti ya dawa

maarufu zinazotumika hapa nchini

ni pamoja na Mchofu, Mvuje,

Mtarawanda, Kivumbasi, Mwavikali

na Mpande ambazo zinatumika

kwa kutibu maradhi mbali mbali

kwa binadamu yakiwemo maradhi

ya tumbo, kichwa, ngiri pamoja

Kima punju ni miongoni mwa rasilimali ya msituni ambayo ni kivutio kikuu cha

Msitu wa Hifadhi wa Jozani kwa watalii wa ndani na wa nje ya nchi.

na maradhi ya matumbo ya

kinamama.

Miti ya mapambo

Miti hii inatumika maalumu kwa

ajili ya mapambo katika maeneo

inayoishi jamii na kupendezesha

hali ya mandhari. Jamii nyingi

zinatumia miti hii katika nyumba

zao au katika sehemu ambazo watu

hupenda kupumzika na kwenye

mahoteli za kitalii. Miongoni mwa

miti maarufu inayotumika kwa

mapambo inayopatikana msituni

ni pamoja na Mgwede, Mkonge,

Mkuyu na Mnunu ambayo pamoja

na kutumika kwa mapambo pia

hutumika kwa kutoa kivuli.

Uhifadhi wa vyanzo vya maji

Maji ni rasilimali za misitu

zinazosaidia uzalishaji wa bidhaa

mbali mbali na kuongeza pato la

taifa na yanasaidia kwa afya ya

binaadamu. Maji ya mito, maziwa,

mvua na sehemu za unyevu ni

vyanzo muhimu vya uzalishaji wa

mazao. Misitu inasaidia kuhifadhi

kina cha maji, kupatika kwa

uhakika na kupunguza chumvi

katika maji. Aidha, miti inatoa nafasi

ya makaazi ya samaki. Majani

na magogo yalioza yanaongeza

virutubisho kwa viumbe waishio

majini.

Rasilimali zinazopatikana msituni

ni muhimu na zinahitaji kuwekewa

mkakati maalum wa kuziendeleza

na kuzitunza kwa vile zinachangia

kustawisha uchumi wa nchi kwa

kuongeza pato la taifa na usitawi

wa maisha ya mwanadamu pamoja

na viumbe vyengine. Aidha, taasisi

zinazohusika ni vyema kufanya

utafi ti na kuweza kuzitangaza

rasilimali hizi na kuzianisha kwa

jamii na matumizi yake.

GAZETI HILI HUTOLEWA KILA BAADA YA MIEZI MITATU NA

WIZARA YA KILIMO NA MALIASILI - ZANZIBAR

P. O. Box 159 Zanzibar, Simu: +255 24 2230986, Fax: +255 24 2234650

Barua pepe: kilimo@zanlink.com, Tovuti: www.kilimoznz.or.tz